SHIRIKA la Omuka Hub kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Marekani National Democratic Institute – NDI wameandaa majadiliano ya jukwaa la wanawake katika siasa kujadili mapendekezo ya kikosi kazi na maazimio ya Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama Vya Siasa yaliyotangazwa 13 Septemba mwaka huu.
Mjadala juu ya ushiriki wa wanawake katika siasa katika ngazi zote kuanzia kitongoji hadi taifa umefanyika Bukoba Mjini na kuhudhuriwa na washiriki 100 kutoka makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo viongozi wa dini, wanawake viongozi , wakuu wa mashirika/NGOs, viongozi wa kisiasa kutoka vyama vya siasa mbalimbali mkoani Kagera kwa lengo la kutoa maoni ambayo yatafanyiwa kazi na kikosi kazi.
Maazimio ya mjadala yanakwenda kuwa chachu katika utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha uwakilishi wa wanawake katika siasa.
Maazimio haya yatawasilishwa kwa kikosi kazi na msajili msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza ambaye alisema mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa ushiriki wa wanawake katika majukwaa ya kisiasa bado upo chini ambapo mwaka 2019 wenyeviti wa vijiji wanaume ni 11,915 wanawake ni 246 sawa na asilimia 2.1,Wenyeviti wa mitaa wanaume ni 4,171 na wanawake ni 528.
Alisema kuwa wenyeviti wa vitongoni wanaume ni 62,612 na wanawake ni 528 huku akisema kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wanawake wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali.
EmoticonEmoticon