Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko kufungua rasmi SHIMIWI

HOJA NEWS BLOG
Na Prisca Libaga, Maelezo

NAIBU Waziri Mkuu na waziri wa nishati, Dkt. Dotto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI), inayofanyika kwenye viwanja mbalimbali mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa SHIMIWI, Alex Temba amesema  mbali na mgeni rasmi wanatarajia uwepo wa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro na viongozi wengine akiwemo mwenyeji Mkuu wa Mkoa Halima Dendego.


 Amefafanua kuwauzinduzi huo utatanguliwa na maandamano ya washiriki zaidi ya 300 yatakayoanzia kwenye Bustani ya TTCL na kumalizikia uwanja wa Samora.


Temba amesema michezo ya mwaka huu imekuwa na mwamko mkubwa kwa timu nyingi kushiriki kwenye michezo ya mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, bao, karata, draft, riadha, darts na kuendesha baiskeli.

“Tuna timu zaidi ya mia na Hamsini kwenye michezo hiyo zinazoshiriki ukiacha mpira wa miguu na netiboli, michezo mingine iliyobaki inashirikisha timu za wanawake na wanaume, hivyo kunaushindani sana,” amesema Temba.

Pia ametoa wito kwa wananchi kuudhuria kwa wingi kwenye uzinduzi huo ambapo pia kutakuwa na mechi za kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume, mchezo wa netiboli na mpira wa miguu.

Katika hatua nyingine michezo iliyochezwa jana katika mchezo wa netiboli timu ya Ofisi ya Rais Ikulu wamewafunga Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa magoli 32-12; huku Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwachapa GST kwa magoli 28-10; nao RAS Lindi wakawaliza wenzao RAS Dar es Salaam magoli 21-18 na Wizara ya Katiba na Sheria wamewachapa RAS Mara kwa 30-12.

Michezo mingine timu ya Ukaguzi waliwaadhibu Wizara ya Mambo ya Nje kwa magoli 66-8; huku Ofisi ya Mashtaka waliwafunga Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA), kwa 17-5; wakati TAMISEMI waliwaliza Wizara ya Ujenzi kwa magoli 29-21.

Katika mchezo wa mpira wa miguu timu zimetoka suluhu, ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi dhidi ya Bohari ya Madawa (MSD); Wizara ya Uchukuzi dhidi ya Tume ya Utumishi na Ofisi ya Waziri Mkuu dhidi ya Wizara ya Kilimo.

Kwa upande wa kuvuta kamba kwa wanawake timu zilizopata ushindi wa mivuto miwili ni pamoja na Wizara ya Kilimo dhidi ya Wizara ya Ardhi; Wizara ya Uchukuzi dhidi ya RAS Simiyu; TAMISEMI dhidi ya Wakili Mkuu wa Serikali; RAS Kagera dhidi ya Wizara ya Mambo ya Nje; na RAS Tanga dhidi ya Katiba na Sheria; wakati zilizopata ushindi wa mvuto 1-0 ni pamoja na Bunge dhidi ya Tume ya Madini; Wizara ya Mifugo na Uvuvi dhidi ya RAS Kilimanjaro.

Kwa upande wa wanaume walioshinda mivuto 2-0 ni pamoja na Mahakama dhidi ya Wizara ya Ardhi; Wizara ya Viwanda na Biashara dhidi ya Katika na Sheria; Ofisiya Rais Ikulu dhidi ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) dhidi ya TARURA.; na walioshinda mvuto 1-0 ni Waziri Mkuu dhid iya RAS Simiyu; 

Katibu tawala msaidizi, seksheni ya Ufuatiliaji na Menejimenti ya Ukaguzi Mkoa wa Arusha Ramadhani Madeleka ,  Ametembelea timu ya klabu ya Ras Arusha mkoani Iringa waliofikia katika hostel ya masista (Irene), na kuwapongeza baada ya kufuzu michuano ya makundi na kuingia  robo fainali.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »