YATANGAZA MATOKEA YA UDAHILI KWA VYUO 287, WASICHANA WAONGOZA KUFIKIA 79%.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufufundi Stadi ( NACTVET ), limeongeza muda wa uhakiki wa Udahili kwa wanafunzi wa programu mbalimbali kwa Mkupuo wa mwezi Septemba 2023 ambapo dirisha hilo la muda wa nyongeza limefunguliwa rasmi leo Oktoba 17, 2023 hadi Oktoba 20, 2023.
Akiongea na waandishi wa habari Jijini Arusha, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko NACTVET, Jeff Shellembi, amesema kuwa NACTVET imeridhia kuongeza muda wa siku 4 wa udahili kwa wanafunzi kufuatia maombi ya vyuo, wadau mbalimbali na wananchi kuomba kuongezwa muda ili wanafunzi wengi wapate fursa ya kujiunga na masomo.
Shellembi ameeleza kuwa muda huo wa nyongeza wa udahili wa wanafunzi ni fursa muhimu pia kwa vyuo kurekebisha na kusahihisha kasoro mbalimbali zilizo jitokeza na pia kuwasilisha wanafunzi waliosahauliwa.
"Hivyo mwombaji anashauriwa kutuma maombi yake kwenye Chuo anachopenda kuanzia leo tarehe 17.10.2023 hadi 20.10.2023 na vyuo kufanya uchaguzi na kisha kuwasilisha kwenye Baraza majina ya waliochaguliwa kuanzia tarehe 18 Oktoba , 2023 hadi tarehe 20 Oktoba, 2023 kwa ajili ya uhakiki", amesema Shellembi.
Ameongeza, "Waombaji walio chaguliwa watafanyiwa uhakiki kuanzia tarehe 21.10.2023 hadi tarehe 23.10.2023 na majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 25 Oktoba,2023 kwa ajili ya kuanza masomo ya mwaka wa masomo 2023 / 2024".
Aidha, NACTVET imevihimiza vyuo pamoja na waombaji kutumia muda huu wa nyongeza kwa makini ili kuepuka usumbufu wowote unaoweza kujitokeza kwa wanafunzi wanaosajiliwa pasipo kuhakikiwa na Baraza.
"Tunapenda kutoa rai kwa vyuo na wanafunzi kuwa makini katika muda huu wa udahili ulioongezwa, na Baraza halitasita kuchukua hatua stahiki kwa chuo kitakachokiuka taratibu za udahili kwa mwaka huu wa masomo 2023 / 2024". alisisitiza Shellembi
Pia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi ( NACTVET ), limetangaza matokeo ya uhakiki kwa wanafunzi waliyo omba kujiunga na programu mbalimbali kwa mwezi Septemba 2023 ambapo udahili huo ulianza Mei 21, 2023.
Shellembi ameeleza kuwa Udahili kwa mwaka wa Masomo 2023 / 2024 ulianza tarehe 21.5.2023 hadi tarehe 16.7.2023 kwa awamu ya kwanza na tatehe 17 hadi 15 Septemba 2023 kwa awamu ya pili ambayo matokeo yao yametoka leo Oktoba 17, 2023, ambapo waombaji walituma maombi yao katika vyuo mbalimbali Tanzania bara na visiwani na kisha kufanya uchaguzi kulingana na sifa za program husika zilizo tolewa na vyuo hivyo.
"Jumla ya waombaji 17,807 kutoka vyuo 287 walichaguliwa na vyuo na kuwasilishwa NACTVET kwaajili ya uhakiki, kuanzia tarehe 3.10.2023 waombaji 16,310 ndiyo waliyo kidhi vigezo vya kujiunga na orogramu walizo chagua na kuziomba ambayo idadi hiyo ni sawa sawa na 91.6% ya waombaji waote, ( Wanawake ni 12,884 sawa na 79% ) na (Wanaume ni 3,426 sawana 21%)". Amesema Shellembi.
"Jumla ya waombaji 1,497 sawa na 8.4% ya waombaji wote hawakuwa na sifa na vigezo vya kujiunga kwenye programu walizo chagua huku wanawake wakiwa ni 726 sawa na 21% na wanaume ni 749 sawa na 50%". Aliongeza Shellembi.
Pia Shellembi ameeleza kuwa waombaji wote waliyo chaguliwa na NACTVET majina yao yameshatumwa vyuoni na wameshatumiwa msimbo ( CODE ) kupitia namba zao simu zilizo wasilishwa na vyuo husika.
"Tumeshatuma majina ya wote waliyochaguliwa vyuoni pamoja na msimbo (code) ambapo msimbo utatumika kuhakiki udahili wao na sifa kwenye programu walizochaguliwa kupitia tovuti ya NACTVET www.nactvet.go.tz kwa kubofya " verfication results 2023". Alisema Shellembi.
"Waombaji waliyochaguliwa na kuthibitishwa wanahimizwa kuwasili kwenye vyuo walivyo chaguliwa na kuhakikisha kuwa wanasajikiwa ili kuanza masomo kama ilivyo pangwa. Pia Vyuo vina agizwa kuwasajili waombaji waliyochaguliwa kwenye mfumo wa Baraza kwa mujibu wa kanuni na taratibu za udahili wa wanafunzi na Endapo chuo kitakiuka taratibu za udahili hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya chuo hicho". Alisisitiza Shellembi.
EmoticonEmoticon