AIRTEL KUBORESHA HUDUMA YA MAWASILIANO YA SIMU NCHINI.

HOJA NEWS BLOG

 Na Prisca Libaga.

Mkurugenzi wa biashara Kampuni ya simu za mkononi, Airtel ,Joseph Muhere, amesema mwaka Jana kampuni hiyo imefunga mtambo mpya Submarinecable ambao ni mkubwa na una uwezo mkubwa wa kupokea na kutumia data kwa kiwango kikubwa ,uwekezaji huo umefanywa kwa ajili ya Watanzania na nchi jirani ambazo zinahitaji mawasiliano kwa njia ya mtandao.

Amesema kuwa kampuni hiyo mwaka huu 2024 inaendelea kufangua huduma  zake za mawasiliano katika miji na Vijiji ambapo kwa mjini kuwezesha kupata huduma ya 3G,4G,5G na Kampuni inaendelea na Uwekezaji na upanuzi wa mtandao maeneo ya Vijiji ili kuwezesha kupata huduma ya 3G 4G na 5G.

Muhere, ameyasema hayo Septemba 18  alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari kwenye kongamano la siku mbili la wadau wa mawasiliano  linalofanyika hoteli ya Gran Melia,Jijini Arusha .

Amesema kuwa lengo la Mkutano huo wa 8 ni kuwaleta Wadau wote pamoja katika teknolojia, ambapo kampuni hiyo inaendelea kuvifikia Vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo ambapo sasa wanajenga huduma ya 5G kwa ajili ya wateja Ujenzi ambao unaenda sambamba na kuhakikisha gharama zinakuwa nafuu.

Mkutano huo wa Connect2Connect Summit umewakutanisha wadau wote wa mawasiliano nchini ikiwemo Airtel Tanzania chini ya kauli mbiu ya ‘Meaningful Connectivity’


Airtel wataonyesha namna gani Mkongo wa Chini ya Bahari wa Airtel 2 Africa utakavyochangia katika maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha mawasiliano kote nchini pamoja na namna ambavyo mkongo huo utasaidia kuiweka Tanzania kama kinara wa kidigitali katika ukanda wa Afrika Mashariki.



Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »