Mwanamume mmoja raia wa Sudan Kusini ambaye anajiita bilionea, amechapisha video kwenye mtandao wa Facebook akionyesha akiwa kwenye kitanda kilichojaa pesa ambazo anadai kuwa ni dola milioni moja
Katika ukanda huo wa dakika nane Lawrence Lual Malong Yor Jn, anazungumza kuhusu vile atatoa pesa hizo kwa kanisa moja iliyo mji mkuu wa Kenya Nairobi. Pia anasema kuwa atatoa pesa hizo kwa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya na nchini Sudan Kusini.
Bwana Malong ambaye pia anajulikana kama Young Tycoon, hasemi vile alipata pesa hizo lakini anasikika akilalamika kuwa watu humkosoa kwa kuonyesa pesa lakini wao husshindwa kutaja misaada yake.
"Mimi ni kama Donald Trump," anasema Malong
Gazeti la Uingerzea la Daily Mail liliripoti kuwa mwaka uliopita bwana Malong alichapisha video nyengine katika mtandao wa Facebook kuonyesha maisha yake.
Daily Mail ilimtaja kuwa mtoto wa kambo wa jenerali mmoj nchini Afrika Kusini.