Al-Shabab "wagawa chakula Somalia''

HOJA NEWS BLOG

Al-Shabab wagawa chakula Somalia
Huku mashirika ya kutoa msaada yakiombia misaada wa dharura kwa waathiriwa wa ukame nchini Somalia, kundi la al-Shabab linasema kuwa limekuwa likigawa chakula kwa wale wanaohitaji.
Al-Shabab wamekuwa wlkipinga vikali kazi ya mashirika ya kutoa misaada nchini Somalia, hata ile ambayo inahusu ukame.
Kundi hilo linayalaumu mashirika hayo kwa kugawa chakula kilicho na kemikali ambazo husababisha magonjwa.
Kwenye taarifa zake kupitia mitandao na redio, kundi hilo sasa linasema kuwa wanamgambo wake wamekuwa wakigawa maji, unga wa ngano, mchele, sukari na mafuta ya kupikia kwa wale wanaokumbwa na ukame nchini Somalia.
Haijulikani ni wapi al-Shabab wanakitoa chakula hicho. Wanadai kuwa wananbunua chakula hicho kutoka kwa masoko lakini huwa wanafahamika kwa kuwotosa ushuru watu na kupora kutoka kwa wanavijiji ambapo watu wanawapinga.
Wakati wa njaa mwaka 2011 , wanamgambo hao walizuia usafirishaji wa misaada na kuwashambulia watoa misaada

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »