Ripoti mpya ya mabadiliko ya hali ya hewa imeonyesha kuwa kuongezeka kwa joto kunaathiri afya ya binaadam kwa kiasi kikubwa.
Ripoti hizo kutoka kundi la vyuo mbalimbali na mashirika tofauti ya umoja wa mataifa zinasema watu wengi wanaathirika na joto pamoja na mlo hafifu sambamba na kusambaa kwa magonjwa.
Katika toleo la Lancet wamesema njaa kwa kiasi kikubwa zinasababishwa na ongezeko la joto linalopelekea mimea kukauka.
Wameonyesha pia uwezekano wa kusambaa zaidi kwa ugonjwa wa malaria kutokana na mazingira kutokuwa saf
WABUNGE wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, leo wamegoma kuhudhuria
kuapishwa kwa Wabunge wapya wa viti maalum kutoka Chama cha wananchi
CUF, kazi iliyofanyika Bungeni na kuongozwa na Spika wa Bunge Job
Ndugai.
Wakiwa wamevalia nguo nyeusi wabunge hao kutoka vyama vyote vya
upinzani bungeni hata wale wa CUF walikuwa katika makundi nje ya Ukumbi
wa Bunge katika jengo la zamani la Ukumbi wa Pius Msekwa.
Baadae baada ya kukamilika uapishaji wa wabunge wapya ndani ya ukumbi
wa Bunge, waliandamana kwa pamoja hadi katika lango kuu la Bunge na
kukusanyika kasha kuzungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi wao
huo wa kugomea shughuli ya kuapisha Wabunge wapya wa kambi hiyo Bungeni.
Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa
Momba, kupitia Chama cha Demorasia na Maendeleo Chadema, David Silinde
alizungumza na wanahabari na kusema kuwa wamefanya hivyo kuunga mkono
wenzao waliofukuzwa na kufungua kesi Mahakamani.
Mwanamume mmoja raia wa Sudan Kusini ambaye anajiita bilionea, amechapisha video kwenye mtandao wa Facebook akionyesha akiwa kwenye kitanda kilichojaa pesa ambazo anadai kuwa ni dola milioni moja
Katika ukanda huo wa dakika nane Lawrence Lual Malong Yor Jn, anazungumza kuhusu vile atatoa pesa hizo kwa kanisa moja iliyo mji mkuu wa Kenya Nairobi. Pia anasema kuwa atatoa pesa hizo kwa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya na nchini Sudan Kusini.
Bwana Malong ambaye pia anajulikana kama Young Tycoon, hasemi vile alipata pesa hizo lakini anasikika akilalamika kuwa watu humkosoa kwa kuonyesa pesa lakini wao husshindwa kutaja misaada yake.
"Mimi ni kama Donald Trump," anasema Malong
Gazeti la Uingerzea la Daily Mail liliripoti kuwa mwaka uliopita bwana Malong alichapisha video nyengine katika mtandao wa Facebook kuonyesha maisha yake.
Daily Mail ilimtaja kuwa mtoto wa kambo wa jenerali mmoj nchini Afrika Kusini.
Bill Gates ampiku Bezos na kuwa mtu tajiri zaidi dunia
Boss Jeff Bezos
alimpiku kwa muda mchache Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani siku
ya Alhamisi kufuatia kupanda kwa hisa za mfanyibiashara huyo kabla ya
ripoti ya mapato yake ,kabla ya hisa hizo kushuka tena.
Mfanyibiashara
huyo ambaye alikuwa nambari nne duniani miongoni mwa watu matajiri
zaidi duniani katika kipindi cha mwanzo wa mwaka alimpiku Bill Gates
mapema siku ya Alhamisi baada ya hisa zake za kampuni ya Amazon kupanda
asilimia 1.8 na kufikia dola 1,071.
Hatahivyo hisa hizo baadaye
zilianguka na hivyobasi kufunga zikiwa zimeshuka kwa asilimia 0.7 kwa
zikiwa dola 1,046, hatua inayoonyesha kwamba Bezos bado hajamshinda Bill
Gates kama mtu tajiri zaidi duniani katika orodha ya jarida la Forbes.
Bezos sasa ana thamani ya dola bilioni 88.5.
Bei hiyo ya
hisa ilijiri saa chache kabla ya Amazon kutangaza mapato ya robo ya
mwaka ambapo ilisema kuwa faida imeshuka kwa asilimia 77.
Hii inatokana na hatua yake ya kuimarisha uwekezaji katika video na upanuzi wa kimataifa.
Gates ambaye ana thamani ya dola bilioni 89.7 amekuwa mtu tajiri zaidi duniani tangu mwezi Mei 2013.
Bilionea huyo ametoa dola bilioni 31.1 ya mali yake kwa mashirika ya hisani.
Kwa upande wake Bezos ametoa ufadhili wa dola milioni 100 pekee kulingana na Forbes.
Bezos amekuwa nyuma ya Gates kwa wiki kadhaa, akiwa na thamani ya dola bilioni 89.3 kabla ya kupanda siku ya Alhamisi.
Mali yake imeongezeka kwa dola bilioni 24.4 mwaka
2017 huku Amazon ambayo inashilikia asilimia 17 ya hisa zikipanda kwa
asilimi 40.
Bezos amempiku bilionea Amancio Ortega ambaye ana
thamani ya dola bilioni 82.7 na Warren Buffet mwenye thamani ya
bilioni 74.5.
Bilionea huyo wa teknolojia alianzisha kampuni ya Amazon 1994 kama duka la vitabu katika gereji yake mjini Seattle.
Amazon sasa ni mojawapo ya kampuni 50 kubwa duniani ikiwa na duka la mtandaoni na vipindi vya runinga.
Ufanisi wa Amazon Prime, umechangia pakubwa ukuwaji wa kampuni hiyo mwaka huu mbali na umaarufu wa Echo Speaker.
Bezos pia inamiliki gazeti la Washington post na kampuni ya safari za angani Blue Origin.
Pia
inamiliki hisa katika kampuni pinzani ya Google, akiwa ndio mtu wa
kwanza kuisadia kampuni hiyo ya utafutaji mbali na Airbnb na Uber.
Baada ya kuwasilia mjini Brussels, Bwana Trump alikutana na mfalme na malkia wa Ubelgiji huku maelfu ya watu wakiandamana kupinga kuwepo kwake mjini Brussels.
Mapewma Trump alikutana kwa muda mfupi na Papa Francis huko Vatican.
Bwana Trump amewalamua wanachama wengine wa NATO kwa matumizi ya chini kwa ulinzi kuliko kiwango kilichoafikiwa cha asilimia mbili ya pato la nchi.
Kabla ya mkutano wa leo Alhamisi , waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Rex Tillerson aliwaambia waandishi wa ahabriu kuwa Trump anataka kuwashinikiza wanachama wa NATO kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Bwana Tillerson alisema kuwa Rais Trump ambaye ameshinikizwa na mataiafa ya Ulaya kuunga mkono mkataba kuhusu hali ya hewa wa Paris, bada hajafanya uamuzi ikiwa Marekani iatajiondoa kwenye makubaliano hayo