Rais wa Marekani Donald Trump yuko mjini Brussels kwa kile kinachotajwa kuwa mazungumzo magumu na wanachama wa Nato.
Trump anatarajiwa kukutana na maafisa wa Ulaya leo Alhamisi. Amekuwa mkosoaji wa NATO na Muungano wa Ulaya.
Baada ya kuwasilia mjini Brussels, Bwana Trump alikutana na mfalme na malkia wa Ubelgiji huku maelfu ya watu wakiandamana kupinga kuwepo kwake mjini Brussels.
Mapewma Trump alikutana kwa muda mfupi na Papa Francis huko Vatican.
Bwana Trump amewalamua wanachama wengine wa NATO kwa matumizi ya chini kwa ulinzi kuliko kiwango kilichoafikiwa cha asilimia mbili ya pato la nchi.
Kabla ya mkutano wa leo Alhamisi , waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Rex Tillerson aliwaambia waandishi wa ahabriu kuwa Trump anataka kuwashinikiza wanachama wa NATO kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Bwana Tillerson alisema kuwa Rais Trump ambaye ameshinikizwa na mataiafa ya Ulaya kuunga mkono mkataba kuhusu hali ya hewa wa Paris, bada hajafanya uamuzi ikiwa Marekani iatajiondoa kwenye makubaliano hayo
EmoticonEmoticon