Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kuna haja ya kukabiliana na itikadi kali katika dini ya kiislamu wakati akitoa hotuba yake nchini Saudi Arabia.
Akiongea kwenye kwenye mji mkuu wa Riyadh, alisema kuwa vita dhidi ya itikadi kali sio vita kati ya imani tofauti bali vita kati ya mambo mazuri na yale maovu.
Trump ambaye yuko kwenye ziara yake ya kwanza katika nchi za kigeni, alizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa kikanda.
Hata hivyo hotuba yake Trump inaonekama kama njia ya kutafuta uungwaji mkono katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic State.
Hatua yake ya hivi majuzi ya kupiga marufuku safari ya kwenda Marekani kwa raia wa mataifa 7 yenye waislamu wengi duniani, ilisababisha hasira kote katika mataifa ya kiislamu
EmoticonEmoticon