Na Prisca Libaga.
Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Hassan Suluhu anatarajia kufungua kikao cha 77 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kitakachofanyika Oktoba 20 hadi Novemba 9 , Nchini Tanzania Jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi Habari Waziri wa Katiba na Sheria,Balozi Dk,Pindi Chana Amesema pendekezo Hilo limekuja Baada ya kuhitimishwa kwa kikao cha Mawaziri cha Kujadili Maandalizi ya Kikao hicho na kuridhiwa kufanyika Hapa Nchi na kutarajiwa kuwaleta wageni zaidi ya 700 kutoka Nchi za Afrika .
Balozi Chana amesema Tanzania imepata sifa ya kufanyika kwa kikao hicho kutokana hali ya utaulivu na Amani ya Nchi sambamba na kuwa mwanachama tangu kuridhiwa kwa mkata wa haki za watu na binadamu na watu 18 Februari 1984 Ambapo kikao hicho kitakuwa na fursa lukuki kwa Nchi na utakuwa niwa siku 21.
Balozi Chana ameendele kutaja Malengo ya kikao hicho mojawapo kikiwa ni maadhimisho ya siku ya hakiza binadamu Barani Afrika kwa kuzingatia itaifaki ya Maputo Msumbiji.
Ametaja masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo maadhinisho ya siku ya haki za binadamu kwakuzingatia itifaki ya Maputo,taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu Barani Afrika,uzinduzi wa nyaraka mbalimbali za kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,taarifa ya wanaharakati wa haki za binadamu na wau,kuidhinishwa kwa itifaki ya mkataba wa Afrika wa Ulinzi wa Jamii.
Lakini pia uwezeshaji wa wanawake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Hali ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na Ukimwi Barani Afriak na Msaada wa Kisheria na Upatikani wa Haki
Kwamujibu wa Balozi Chana alisema mkutano huo unahisisha sekta mbalimbali ikiwemo masuala ya kimataifa,utamaduni,sanaa na michezo,fedha na uchumi,ulinzi na usalama ,afya ,habari na mawasiliano.
MWISHO.
EmoticonEmoticon