EDWARD LOWASSA NI MWAMBA WA KASKAZINI

HOJA NEWS BLOG

Na Novatus Makunga.

Leo Ijumaa ya tarehe 16 Februari 2024 ndiyo siku rasmi ya kutoa heshima ya mwisho kwa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa kijijini kwake Ngarash wilayani Monduli Mkoani Arusha.

Ni nafasi pekee kwa wananchi wanaoishi mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni pamoja na Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Nianze kwa kueleza kuwa mwanzoni baada ya kutangazwa kwa msiba huo mkubwa nchini katika andiko la kwanza kabisa nilitu.


mia Mwamba wa Kaskazini lakini wadau wakanikosoa na kuja na hoja kwamba Mzee hakuwa Mwamba wa kaskazini bali Ni Mwamba wa Tanzania na wengine wakaenda mbali kuwa ni Mwamba wa Afrika ya Mashariki. Wote walikuwa na hoja zenye mashiko hivyo nawakubaliana nao Mzee Edward Lowassa ni MWAMBA. 

Mwamba, kwangu mimi kwa mara ya kwanza nilibahatika kufahamiana naye mwaka 1993. Nilikutana naye katika kazi nikiwa Mwandishi wa habari mchanga mno.

Mwamba wakati huo alikuwa Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro.

Nilivutiwa sana na uwezo wa akili yake katika kuchanganua mambo.

Mwenyeji wake alikuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro(RC) wa wakati huo Marehemu Samuel Sitta. Tulitoka Arusha na kaka yangu katika tasnia Noel Thomas, yeye akiwa mzoefu. 

Ilikuwa bonge ya ziara kwani kazi ilikuwa ngumu lakini habari kwa maana 'story' za kuipasha jamii zilipatikana, lakini kikubwa tulikuwa na viongozi makomredi katika siasa na wapambanahi ambao kwa wakati huo walikuwa 'moto wa kuotea mbali* 


MWAMBA LOWASSA ZAIDI YA UNAVYOMFAHAMU

1.Mwamba kwa  siasa za Tanzania alikuwa ni mwanasiasa bora wa wakati wote 'All Seasons Politician'.Ni Mtu bingwa sana wa siasa za kimikakati ambaye alikuwa tishio kwa washindani wake kisiasa. Alikuwa mtaalamu katika  siasa za Majukwaani. Mwamba alijua aseme nini na wapi kulingana na hadhira.Mwamba alikuwa mwanasiasa aliyehakikisha hatengenezi mahasimu wa kisiasa bali alijitahidi hata  maadui zake kisiasa kuwa marafiki 

2. Ni vigumu mno kumsahau mtu. 

Mwamba alikuwa na sifa moja kubwa ya kutomsahau mtu kwa sura na jina. Ilikuwa ni ajabu katika ziara iwe Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga au Mtwara ama kona yoyote ya nchi katika ziara zake.Mwamba alikuwa anawatambua kwa majina mpaka maofisa tarafa au wenyeviti wa vijiji.

3. Kuwajali na kuwathamini anaofanyanao kazi. 

Mwamba alikuwa na tabia ya kuhakikisha anaofanya nao kazi wapo kwenye 'Comfort Zone'. Ni marufuku kuwa na kero zisizo na msingi, mfano kwa waandishi wa habari. Mwamba katika ziara zake alikuwa yupo radhi tukutane naye hata saa sita usiku kwa ajili ya tathimini ya ziara na siku ya pili ziara ikaendelea kwa kuanza kwa muda uliopanga mapema alfajiri. 

4.Chanzo Kikubwa cha habari

Kwa Mwandishi wa habari yeyote kupata habari nzito ambayo itayopendwa na jamii ndiyo kipaumbele na hapo Mwanahabari anakuwa salama. Mwamba alikuwa na sifa kubwa ya kuwa chanzo cha 'story' kubwa sana na ambazo zinatikisa. Kwa msingj huo alikuwa kiongozi pekee wa kisiasa nchini aliyekuwa karibu sana na rafiki mkubwa wa Wanahabari. 

5. Mtu wa Hoja zaidi kuliko nguvu. 

Mwamba Kama mwanasiasa alikuwa mtu wa mikakati ambaye alihakikisha kila hoja kinzani inapata majibu sahihi kwa muda muafaka. Waandishi wa habari tulikuwa tunafahamu ukitaka kuvuka "Yellow Ribbon" yake jiandaye kubishania hoja ukimshinda anakuwa mpole lakini atakupa mtazamo wake. Ni kiongozi pekee wa ngazi yake ambaye  unaweza kumpata kwa njia ya simu kwa muda wowote. Hii ina maana anapokea simu tofauti na viongozi wengi. 

ASANTE MWANBA LOWASSA, PUMZIKA KWA AMANI

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »