'Adui wa mwanamke ni mwanamke', ni msemo ambao umekuwa ukitumika mara kwa mara. Mara nyingi una lengo la kueleza kuwa anayekwamisha maendeleo ya mwanamke ni mwanamke mwenyewe

HOJA NEWS BLOG
Stella Radini wa nchini Tanzania ni mama wa watoto wawili anayefanya kazi ya udereva wa magari makubwa yafanyayo safari za masafa marefu kwa takriban miaka 16 sasa.
Yako mambo kadhaa yanayoyatajwa ikiwemo kuibiana ama kugombea wanaume, fitina, ugomvi wa mawifi, kupeana ushauri mbaya wa kumgombanisha mwanamke na mumewe, kunyimana fursa kwenye kazi kwa mfano bosi wa kike kumnyima fursa mwanamke mwenzake, wivu na tamaa.
La zaidi pia kuna dhana kuwa wanawake wanapotofautiana kimawazo au kwa namna yoyote ile, ugomvi wao huchukua muda zaidi kuisha huku wakihusisha watu wengine juu ya yule waliyetofautiana naye tofauti na wanaume ambao mara nyingi wanatajwa kutokuwa na kinyongo kwani hata wanapofarakana tofauti zao huisha haraka bila kuhusisha watu wengine.
Kwa mujibu wa waandishi mbalimbali wa mambo ya kijamii, mara kwa mara wanawake ndio wamekua wakishindana wenyewe kwa wenyewe hali inayosababisha kurudishana nyuma kwa sababu mbali mbali.
wanawakeHaki miliki ya pichaAFP

Wivu na uchoyo

Katika chapisho la mwaka 2014, "Women are their own worst Enemies" kwa tafsiri isiyo rasmi likimaanisha 'Mwanamke ni adui wa mwanamke' lililoandikwa na Lucille Keen, anasema "wakati wanaume wanapandishiana sauti na mara nyingine kuishia kukunjiana ngumi, wanawake kisirisiri wanarudishana nyuma taratibu kwa kutesana kisaikolojia. Sio kwa sababu tunafikiri wanawake wengine hawawezi, ila kwa sababu tunawaona kuwa ni tishio."
Inasemekana kuwa mwanamke anapomfanyia ubaya mwanamke mwenzie hufanya kwa kificho kutoka moyoni.
"Haya mapambano yanafanyika kisirisiri na katika visa vingi yanafanywa na wanawake hao hao wanaoimba na kusifu nguvu ya mtoto wa kike, harakati za mambo ya wanawake na wanawake kupendana,"anasema Kelly Valens, kupitia kitabu chake cha "The twisted sisterhood" cha mwaka 2010.
Katika utafiti wake, kwa wanawake zaidi ya elfu tatu, Valens anasema asilimia 90 ya waliohojiwa wanasema wamefanyiwa roho mbaya ama uchoyo na wanawake wenzao. Takribani asilimia 85 wanakiri kuwa wamekabiliwa na vitendo vya kutishiwa maisha wakiwa mikononi mwa wanawake wenzao na zaidi ya asilimia 75 wanasema wameumizwa na wivu pamoja na ushindani toka kwa marafiki zao.
Jokate Mwegelo
Image captionSio wote walioukubali uteuzi wa Jokate Mwegelo mkuu mpya wa Wilaya Tanzania huku baadhi wakihoji uwezo wake kuhudumu katika wadhifa huo, miongoni mwao wanawake
Kupitia utafiti huo, Vallens anasema wanawake hao kwa usahihi wamethibitisha kuwa tishio la kwanza kwa hisia za mwanamke ni mwanamke mwenzake.
Hata hivyo tafsiri ya tabia ya mwanamke mara nyingi hutolewa na namna mwanamke anavyotazamwa na jamii. Mara nyingine ni jinsi wanaume wanavyomuona au hata waajiri wanavyomchukulia na pengine anavyoelezewa katika sekta tofauti za jamii kama siasa, elimu, afya na biashara.

Kutegemea msaada kutoka kwa wanaume

Ili kupata mitazamo tofauti, BBC imezungumza na Naibu msajili wa mahakama kuu Tanzania Bi Nyigulila Mwaseba anayesema chuki ni tabia ya mtu tu bila kujali jinsia.
"Si kweli, hii huenda inatokea kwa sababu mtu alitegemea kupata huduma au kusaidiwa na mwanamke mwenzake alafu akakosa hicho alichohitaji ndio mtu husema hivyo. Kwa msimamo wangu naamini mtu yeyote yule anaweza kuwa mwanamke au mwanaume akakufanyia visivyo, anaweza kuwa bosi wako ama vyovyote. Ni moyo wa mtu tu mwenyewe.
Nyigulila MwasebaHaki miliki ya pichaNYIGULILA MWASEBA
Image captionNyigulila Mwaseba - Naibu msajili wa mahakama kuu Tanzania
"Kama mtu hana roho nzuri ni yeye tu kwa sababu unaweza kuhudumiwa vizuri na mwanamke mwenzako na ukaudumiwa vizuri na mwanaume pia hii haijalishi. Binafsi naamini ni tabia tu binafsi," anasema Bi Mwaseba.
Hata hivyo anawashauri wanawake hasa wanaokwenda kwenye maofisi mbali mbali kuacha kwenda mahali wakiwa na mategemeo kuwa wakimkuta mwanaume basi watahudumiwa vizuri au ukimkuta mwanamke mwenzako utahudumiwa vizuri. Anasisitiza si vyema kwenda na matarajio.
"Iwapo umeenda kupata huduma au msaada mahali na mtu uliyemkuta hajakupatia huduma kama inavyotakiwa unaweza kufuata utaratibu wowote ambao utafuata hata kama umemkuta mwanaume na si mwanamke," anaongeza Mwaseba.
Lakini kukinzana mawazo si jambo la kushangaza mwingine anaona ni wivu baina ya wanawake.
Josephine MaximeHaki miliki ya pichaJOSEPHINE MAXIME
Image captionJosephine Maxime Mwanahabari Tanzania

Wanaume ndio chanzo?

Mwanahabari Josephine Maxime ana mtazamo tofauti na ule wa Bi Mwaseba.
"Wanawake wanapotetea haki yao wanakuwa na umoja sana, lakini linapokuja suala la haki na maendeleo ya mwanamke mmoja mmoja, wivu unaanza kuibuka na majungu na fitina, mfano mwanamke mwenzao apate cheo kazini ni shida watashindana, uzuri, kipato na hata kwenye kugombea uongozi wako tayari kumpa mwanaume kuliko mwanamke mwenzao," anasema mwanahabari Bi Josephine Maxime.
Hata hivyo baadhi ya wanawake wanaona msemo huu ni propaganda inaendekezwa na wanaume ili wanawake wachukiane wao kwa wao.
"Hii propaganda imefanya kazi sana wanawake tuonane wabaya na yote hiyo ni kwa manufaa ya wanaume," anasema Irene Joseph
BBC imezungumza na Shahista Alidina maarufu kama Shaykaa, mwanaharakati wa haki za binadamu. Kwake, tatizo lipo kwa baadhi ya wanawake kukosa kujiamini.
"Unaweza kuta mwanamke amesoma mzuri na ana kila kitu lakini tatizo linakuja kwenye kujiamini, kama unajiamini mwenyewe huwezi kuwa na chuki na mwenzako hata awe amekuzidi vipi kwa sababu unakuwa umejitosha na umeridhika na ulicho nacho na ulivyokuwa sio mwenzio anafanya vizuri unaanza kwanini huyu anaendelea kuliko mimi wakati amekuja juzi tu," anasema Shaykaa.
Hata hivyo Shaykaa anasisitiza kuwa wapo wanawake wengi wanapendana na wanaleta maendeleo kwa pamoja. Na anasisitiza mwanamke ni kujipenda na kujiamini kwani ukiwa hivyo hutapata muda wa kuwa na chuki na mtu.
Shahista AlidinHaki miliki ya pichaSHAHISTA ALIDIN
Image captionShahista Alidin anasisitiza kuwa wapo wanawake wengi wanapendana na wanaleta maendeleo kwa pamoja

Adui na mshindani

Ni mjadala mkubwa, BBC imezungumza na mwanasaikolojia Sreddie Kyara ambapo yeye anasema kuna tofauti ya adui na mshindani.
"Kisaikolojia nikitazamia adui ni mshindani, naweza kusema mwanamke ni adui mkubwa wa manamke na kwasababu hasa mwanamke hutaka kushindana na zaidi na mwanamke kuliko mwanaume kwa hiyo hii ndio inapelekea kufanya mwanamke kuwa adui mkubwa wa mwanamke kuliko mwanaume kuwa adui wa mwanamke," anasema Kyara.
Hata hivyo anasisitiza kuwa maumivu mengi ya wanawake husababishwa na wanawake wenzao pamoja na kwamba wanaume hushiriki. Anatolea mfano wa mahusiano kuwa mwanamke huyu huyu anatembea na mume wa mwenzie akijua wazi kuwa mwanamke mwenzake ataumia na kuteseka.
"Kama wanawake wangeungana wakasema wanataka kukomesha mateso wanayopitia wangefaulu sana. Lakini kwa sababu mateso mengi wanawake wanayopitia ni kwa sababu wanawake hao hao wanaruhusu wanaume kuwafanyia wanawake wenzao ni ngumu," anaongeza Kyara
Hata hivyo mwanasaikolojia huyo amewataka wanawake kuamka ili kumaliza ushindani na wakati huo huo amewasifu wanawake kuwa wana bidii ya kusaidiana.
"Wanaowasaidia wanawake kwa asilimia kubwa ni wanawake na kwa msaada ambao ni halisia ni wanawake kuliko wanaume, lakini pia wanawake watambue kuwa atakayeweza kumuinua mwanamke ni mwanamke mwenyewe na atakayeweza kumwangusha mwanamke kwa nguvu zaidi si mwanaume ni mwanamke mwenzake," Kyara ameiambia BBC.
Bila shaka huu ni mjadala mzito ambao ni vigumu kufikia tamati, wewe una maoni gani?

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »