Na Prisca Libaga Maelezo, Arusha
kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii imepongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga sh. bilioni 8 kwa ajili ya kutelekeza mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) ardhi katika eneo lililopo pembezoni mwa Uwanja wa Michezo wa Afcon unaojengwa kata ya Olmort Jiji la Arusha.
Pongezi hizo zilitolewa jana Jijini Arusha na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Najma Murtaza Giga wakati kamati hiyo ilipotembela na kujionea eneo la mradi wa KKK pamoja na kujionea ujenzi wa uwanja wa Afcon unaojengwa kwa ajili ya mashindano ya mpira mwaka 2027.
Aliipongeza serikali kupitia Wizara ya Ardhi kwa kuja na mradi huo wa viwanja na kuongeza kuwa tukio hilo ni la kihistoria kwani ndani ya miaka miwili ya ujenzi wa uwanja huo wa Afcon si mbali hivyo serikali iharakishe ujenzi huo huko makazi ya wananchi yakipimiwa na kuanishwa shughuli mbalimbali za maendeleo.
"Hii ni historia na Arusha ina historia yake kwa utalii na fursa zingine hivyo tunahitaji taarifa kamili juu ya mradi huu ili tuweze kuishauri serikali katika kuhakikisha vipaumbele vya awali vinapatikana na fursa za uwekezaji zinakuwepo kwani Afcon haipo mbali lazima tujipange kwani eneo hili la viwaja si mbali na mji na Jiji la Arusha litapendeza sana mara mradi huu utapokamilika"
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi alisema fedha hizo zimetolewa na wizara hiyo kwa ajili ya ulipaji wa ekari 207 za awali kati ya ekari zaidi ya 4,575.5 zilizopo katika mpango wote huo ambapo uwanja wa Afcon pekee unakeri 83 .
"Wizara imetenga fedha hizi kwa ajili ya kuanza ulipaji fidia na tunategemea tukimaliza kupima viwanja hivi tutanunua vingine hapo badae kadri wizara itakavyopata fedha kwaa ajili ya kupima, kupanga na Kumilikisha lengo letu mji wa Arusha na maeneo mengine nchi nzima yapangwe badala ya kuwa na maeneo yasiyopangwa"
Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Pinda alisema Arusha ni mji wenye historia ya aina yake hivyo lazima mipango sahihi iwepo katika kuondoa mji katika maeneo yasipoangwa hadi iwe iliyopangwa na kuwasihi wananchi wa mkoa huo wawe na subra wakati serikali ikipanga mji huo na kuipongeza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuhakikisha mji unapangwa na kuwa na Maendeleo zaidi.
"Tupo makini kuhakikisha mji unajengwa na uwanja wa Afcon ukiisha hapa tutakuwa na makazi yenye mpangilo bora na wa aina yake"
Huku Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye ni mbunge kutoka Tabora, Emmanuel Mwakasaka alipongeza wizara hiyo kwa kuja na mkakati huo wa upimaji maeneo nchi nzima na kumshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja huo wa Afcon ambao utawezesha Mkoa wa Arusha kupaa zaidi kimapato.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo wa upimaji Ofisa Mipango Miji Halmashauri ya Arusha Dc, Georgia Mwamengele alisema wizara ipo katika katika mchakato huo ili kuwezesha miji wa Arusha kupangwa na kuanza kuondoa makazi holela.
Mwisho